Our City
🏛 Historia ya Mji Mkongwe
Asili na jina: Mji Mkongwe unajulikana pia kama Stone Town kwa Kiingereza. Ni sehemu ya kale ya Zanzibar mjini, kisiwa cha Unguja.
Ujenzi wa awali: Nyumba nyingi zilianza kujengwa kuanzia mwaka 1830, baada ya Sultani Sayyid Said kuhamisha mji mkuu wake kutoka Oman kuja Unguja.
Mchanganyiko wa tamaduni: Mji huu ulijengwa kwa ushawishi wa Waarabu, Waajemi, Wahindi na Wazungu, jambo linaloonekana katika usanifu wa majengo, milango yenye mapambo, na mitaa yenye historia ndefu.
Urithi wa Dunia: Mji Mkongwe umeorodheshwa na UNESCO kama sehemu ya World Heritage Site